Radi yaua na kujeruhi wanafunzi Shule ya Sekondari Businda

GEITA-Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa pole kwa wananchi wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita kufuatia ajali ya radi iliyotokea leo Januari 27, 2025 katika Kata ya Ushirombo.
Sehemu ya taarifa hiyo salamu za pole ya Dkt. Biteko iliyotolewa leo Januari 27, 2025 inaeleza kuwa ajali hiyo ya radi imesababisha vifo vya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Businda.

“Nimepokea taarifa ya vifo vya watoto wetu wa Businda Sekondari kwa masikitiko makubwa. Naomba kuwapa pole sana wazazi, walezi, walimu, wanafunzi wa shule hii na ndugu wote waliguswa na msiba huu mkubwa,” amesema Dkt. Biteko.

“Vifo vya vijana wetu vimetushtua sana wana Bukombe wote. Tunawaombea faraja familia zote zilizofikwa na msiba huu aidha, tunawaombea uponyaji wa haraka majeruhi wote kwenye kadhia hii.”

Aidha, Dkt. Biteko ameelekeza Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Ofisi ya Mbunge kufuatilia kwa karibu matibabu ya majeruhi wote na taratibu za mazishi ya wanafunzi hao walioaga dunia.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Mhe. Paskasi Muragili akizungumza na wananchi mbalimbali waliokusanyika eneo la Hospitali ya Wilaya ya Bukombe amesema, “Tukio la ajali ya radi imesababisha vifo 7 kwa wanafunzi na kujeruhi wanafunzi 82 ambapo wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali yetu ya wilaya.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news