Radi yaua ng'ombe 10 wakiwa malishoni

RUKWA-Zaidi ya ng'ombe 10 wamekufa papo hapo, baada ya kupigwa na radi katika Kijiji cha Mwenge kilichopo Kata ya Kate wilayani Nkasi wakiwa malishoni.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kate, Deus William Njugu amesema,ng'ombe hao walipigwa na radi majira ya saa 9 alasiri wakiwa malishoni na wakati radi hiyo inapiga palikua na ng'ombe 15 na wote walindondoka chini.

Njugu alisema,baada ya muda ng'ombe 5 walisimama na kuondoka huku 10 wakipoteza maisha.

Alisema kuwa,katika ng'ombe hao waliokufa watano ni madume na watano ni majike na kuwa ng'ombe hao wote ni mali ya Steven Slanda mkazi wa Kijiji cha Mwenge.

Amefafanua kuwa,ng'ombe hao wote baada ya kufa kwa radi hiyo walianza kujaa matumbo,huku kijana aliyekua akiwachunga ng'ombe hao akiwa salama.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwenge,Charles Kafumu alikiri kutokea kwa tukio hilo na kila mwaka inapofika msimu wa mvua za masika ni lazima radi ipige na kusababisha madhara kwa jamii kama hayo ya kuuliwa kwa mifugo na hata binadamu au vyote kwa pamoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news