Rais Dkt.Mwinyi aendelea kuipaisha Pemba, barabara za kisasa zinajengwa kwa kasi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia wananchi wa Pemba kuwa, barabara nyingi kisiwani humo zitajengwa kwa kiwango cha lami.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo alipozindua Barabara za Kilomita 10 za Micheweni-Kiuyu-Maziwa Ng'ombe na Barabara ya Michweni -Shumba Mjini hadi Bandarini Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Aidha,amefahamisha kuwa Serikali ina Programu Maalum ya Kuziwekea Taa Barabara zote zilizojengwa kwa kiwango cha lami nchi nzima.

Rais Dkt.Mwinyi amewahimiza wananchi kuacha kujenga katika hifadhi za barabara kwani zimetengwa maalum kwa ajili ya kuendeleza miundombinu mingine.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, kumekuwa na tabia ya watu kujenga pembezoni mwa barabara kwa kutegemea kulipwa fidia na Serikali jambo ambalo sio sahihi.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amezitaka halmashauri kusimamia suala hilo na kudhibiti utoaji wa vibali holela vya ujenzi pembezoni mwa barabara.
Akiwasilisha Taarifa ya Kitaalamu ya Ujenzi wa Barabara Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dkt.Habiba Hassan amesema,ujenzi wa barabara hizo zenye urefu wa kilomita 10 ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2025,Dira ya Maendeleo ya Zanzibar, Mpango Mkuu wa Maendeleo wa Taifa na Mpango Mkuu wa Usafiri ambapo Barabara zenye Urefu wa Kilomita 140.9 zimejengwa Unguja na kilomita 134.9 zimejengwa Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news