Rais Dkt.Mwinyi afungua nyumba 72 za makazi na biashara Mombasa kwa Mchina

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewathibitishia wananchi kuwa,Serikali itaendelea kujenga nyumba za kisasa maeneo yote ambayo yana nyumba chakavu kwa lengo la kuwapatia wananchi makazi bora.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa nyumba 72 za Makazi na Biashara Mombasa kwa Mchina Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHC).

Rais Dkt.Mwinyi ameiagiza Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuandaa Mpango Maalum wa Kisheria wa Matunzo ya Nyumba inazozijenga ili suala la matunzo kuwa la lazima na sio hiyari.
Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa, mpango huo ni lazima uzingatie Mifumo ya Maji, Masuala ya Usafi na Uangalizi wa Nyumba zenyewe ili ziendelee kuwa na haiba nzuri ilizonazo hivi sasa.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewashauri wamiliki wa nyumba hizo kuanzisha Kamati Maalum za Matunzo ya Nyumba hizo kwa kila mmiliki kuwajibika na usafi na matunzo ya nyumba anayomiliki.

Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kuwa,wananchi ni lazima wakubali kupisha Miradi ya Ujenzi wa Nyumba na kwamba Serikali itawafidia nyumba nora za makazi badala ya fedha.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa wananchi kukaa katika makazi mazuri ndio dhamira ya Serikali na kuwa Mpango wa Ujenzi wa Nyumba 3,000 eneo la Chumbuni utaendelea katika maeneo mengine na kuwaambia wakazi wa Kikwajuni kukaa tayari kwani nyumba 500 zitajengwa katika eneo hilo na Serikali ipo tayari kwa mradi huo.
Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuridhika na utendaji wa wizara hiyo kwa mafanikio makubwa ya miradi ya ujenzi wa nyumba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news