Rais Dkt.Mwinyi afungua Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini,awaondoa wananchi hofu wanaozusha madeni ya nchi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia wananchi kuwa Serikali inatenga kiasi cha dola za kimarekani milioni 10 sawa na shillingi bilioni 300 kwa mwaka kwa ajili ya kulipa madeni ya nchi.
Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa,wakati Serikali inakopa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo Ina Akaunti Maalum inayoweka fedha za kutosha kulipa madeni hayo ambayo sasa ina kiasi cha shillingi biliioni 600.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipofungua Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini,Mkoa wa Mjini Magharibi kilichojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF).
Amefahamisha kuwa,deni ililonalo Zanzibar kwa sasa ni shillingi trilioni 1.2 linaloaminika na kuwa na uwezo wa kukopesheka tena kutokana na utaratibu huo uliopo Serikali inaweza kulilipa kipindi cha miaka miwili.

Aidha,ameeleza kuwa wakati Serikali ya Awamu ya Nane inaingia madarakani deni la Serikali lilikuwa Shillingi Bilioni Mia nane na sasa baada ya miaka minne limepanda hadi kufikia trilioni 1.2.

Rais Dkt.Mwinyi amekanusha vikali taarifa zilizotolewa na Wapinzani hivi karibuni kuwa Zanzibar ina deni linalofikia Trilioni 2.8 sawa na ongezeko la asilimia 208 kuwa za Uongo na Propaganda za Kisiasa zisizo sahihi.

Amesisitiza kuwa,Serikali inakopa kwa nia njema ya Kuendesha Miradi ya Maendeleo yenye tija na maslahi kwa nchi na sio vinginevyo.

Akizungumzia kituo hicho kipya cha Mabasi ameutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZSSF kuwa na Mpango maalum wa Matunzo na Usafi na kuandaa ajira Maalum kwa Vijana kwa ajili kutoa huduma hizo.

Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa Serikali inakuja na Mpango Mkuu wa Usafiri utakaoifanya nchi kuwa na Usafiri wa Kisasa na Huduma Bora.
Mpango huo utajumuisha Ujenzi wa Vituo vya Kisasa vya Mabasi katika Maeneo ya Chuini, Jumbi, Mwera na Mwanakwerekwe pamoja na Kijangwani ,Malindi na Mnazi Mmoja kwa Eneo la Mjini kusisitiza kuwa kabla Mwisho wa Mwaka huu Zanzibar itaanza kutumia Mabasi ya Umeme.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news