Rais Dkt.Mwinyi afungua Skuli ya Sekondari Tumbatu

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameifungua skuli ya kwanza ya ghorofa Kisiwani Tumbatu iliyogharimu shillingi bilioni 7.015.Akizungumza na wananchi baada ya kuifungua Skuli hiyo Rais Dkt.Mwinyi ameziagiza mamlaka zinazoshughulika na ajira kuhakikisha zinatoa fursa za ajira kwa vijana wa Tumbatu wenye sifa zinazohitajika.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipoifungua Skuli ya Sekondari ya Tumbatu wilaya ndogo ya Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amezitaka mamlaka hizo katika Sekta za Afya,Elimu, Miundombinu, Maji, Umeme na nyinginezo kusimamia agizo hilo ili miradi iliyopo Tumbatu ilete tìja kwa wananchi na kuongeza ufanisi.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa,Serikali inakusudia kujenga nyumba za walimu na dahalia ili walimu watakaofundisha katika Skuli ya Tumbatu waishi katika nyumba hizo.

Rais Dkt.Mwinyi amewahakikishia wananchi wa Tumbatu kuwa kinachofanyika sasa ni utekelezaji wa ahadi zake na kwamba zitaendelea kutekelezwa zaidi.Akizungumzia suala la utalii ameeleza kuwa, Serikali haina nia ya kupeleka shughuli za utalii kisiwani humo na kuwataka wananchi kuyaepuka maneno yasio na ukweli yanayoenezwa na watu wasiopenda maendeleo.

"Sina nia ya kuleta utalii Tumbatu, utalii utapelekwa kwa watu wanaoutaka sio Tumbatu,"alisisitiza Dkt.Mwinyi.
Rais Dkt.Mwinyi amewahimiza vijana kusoma kwa bidii kwa lengo la kuongeza ufaulu kufuatia kuwepo kwa Skuli yenye viwango vya ubora,maktaba,maabara ya kisasa ya Sayansi na madarasa mazuri.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ameliagiza Shirika la Umeme kuondoa changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara,tatizo alilolielezea kuwa ni la nchi nzima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news