ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesaini Kitabu cha Maombolezo Ubalozi mdogo wa India uliopo Migombani, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa India, Hayati Manmohan Singh kilichotokea Desemba 26,2024.
Rais Dkt.Mwinyi aliwasili Ubalozini hapo leo Januari 1,2025 na kupokewa na Balozi mdogo wa India Mhe.Dkt.Kumar Praveen.
Hayati Manmohan Singh aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa India kuanzia mwaka 2004 hadi 2014.