ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kwa waumini kuweka mkazo katika kusoma na kutoa elimu ya dini kwa dhamira ya kunusuru jamii na changamoto zinazowakabili.
Alhaj Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika sala ya Ijumaa na kuufungua Msikiti mpya wa Chanjaani Mwanamashungi Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Pia,amesema kuwa ni vema misikiti ikatumika kwa kusali,kusoma pamoja na kuitunza ili iwe na mazingira mazuri kwa ibada.
Aidha, amewanasihi waumini wa Dini ya Kislamu kuitumia nisikiti vizuri kukabiliana na changamoto katika jamii.
Kwa upande mwingine,Alhaj Dkt.Mwinyi amewahimiza waumini wa dini ya Kislamu,viongozi wa dini na wanasiasa pamoja na waandishi wa habari kuhubiri amani zaidì wakati nchi ikielekea katika Uchaguzi Mkuu.