ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar,Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika kusherehekea miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar amewapa msamaha na kuwaachia huru wanafunzi 33 wanaotumikia adhabu zao Chuo cha Mafunzo Zanzibar.