Rais Dkt.Mwinyi awashukuru wasanii kwa kumuunga mkono

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru wasanii wote kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi,  tangu ameingia madarakani wamekuwa wakijitolea kufikisha ujumbe kupitia sanaa ya burudani na kuitangaza Zanzibar.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Rais na Mmiliki wa Crown Media, Ali Saleh Kiba na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar leo Januari 24,2025.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano wasanii wote katika shughuli mbalimbali.

Naye Ali Saleh Kiba amemuahidi Rais Dkt.Mwinyi kujitolea bega kwa bega kutangaza mafanikio ya Zanzibar kupitia sanaa yake ya muziki na kituo chake cha habari cha Crown Media kuwapa habari wananchi kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news