Rais Dkt.Mwinyi awasili Dodoma

DODOMA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi ameondoka Zanzibar nankuwasili jijini Dodoma kwa ajili ya shughuli za kikazi.
Katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma, Rais Dkt.Mwinyi amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi akiwa Dodoma atashiriki vikao vya kikatiba vya Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Taifa vikiwemo Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025 jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news