Rais Dkt.Samia afanya mazungumzo na Mratibu Mkazi wa UN nchini
DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi. Susan Namondo, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 13 Januari, 2025.