NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani wanne.
Miongoni mwao ni Jaji Latifa Alhinai Mansoor ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi, Morogoro na Jaji George Mcheche Masaju ambaye kabla ya uteuzi hu alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mshauri wa Rais, Sheria.
Wengine walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni Jaji Dkt. Deo John Nangela ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga.
Sambamba na Jaji Dkt. Ubena John Agatho ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam.
Wakati huo huo,Rais Dkt.Samia amempangia Balozi Dkt. Stephen John Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil akichukua nafasi ya Balozi Prof. Adelardus Kilangi ambaye amepangiwa majukumu mengine.
Vilevile,Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Uledi Abbas Mussa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kipindi cha pili.
Aidha,Rais Dkt.Samia amemteua pia Prof. Zacharia Mabubu Mganilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) akichukua nafasi ya Prof. Wineaster Anderson ambaye amemaliza muda wake.