DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Dkt. Moses Kusiluka walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
(i) Jaji Mstaafu Beatrice Rhoda Mutungi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Rufani za Kodi (TRAT).
Jaji Mstaafu Mutungi anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Gad John Mjemmas ambaye amemaliza muda wake;
(ii) Dkt. Diwani Bakari Msemo ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi yaSaratani Ocean Road (ORCI).
Dkt. Msemo ni Daktari Bingwa wa Magonjwa yaSaratani, anachukua nafasi ya Dkt. Julius David Mwaiselage ambaye atapangiwa majukumu mengine; na
(iii) CPA. David Carol Nchimbi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NMB Plc.
CPA. Nchimbi anachukua nafasi ya Dkt.Edwin Mhede ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.