Rais Dkt.Samia afanya uteuzi Tume ya Madini,FCC,TBS,TFC na CAMARTEC

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt.Moses Kusiluka walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

(i) Mhandisi Ramadhani Masoud Lwamo ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Lwamo alikuwa akikaimu nafasi hiyo;

(ii) Dkt. Aggrey Kalimwage Mlimuka ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ushindani (FCC) kwa kipindi cha pili;

(iii) Prof.Othman Chande Othman ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kipindi cha pili;

(iv) Dkt.Florens Martin Turuka ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kwa kipindi cha pili; na

(v) Prof. Valerian Cosmas Silayo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kwa kipindi cha pili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news