NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, uhamisho na mabadiliko ya viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka uteuzi, uhamisho na mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:
a) Wakuu wa Wilaya
(i)Bw. Godfrey Eliakimu Mnzava, Afisa Tarafa ya Ilemela ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. James Wilbert Kajialiyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA);
(ii)Bw. Michael John Semindu, Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa ameteuliwa kuwaMkuu wa Wilaya ya Mbulu kuchukua nafasi ya Bi. Veronica Arbogast Kessy ambaye amestaafu;
(iii) Bw. Khamana Juma Simba, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha ameteuliwa kuwaMkuu wa Wilaya ya Ulanga kuchukua nafasi ya Dkt. Julius Keneth Ningu ambaye amestaafu;
(iv) Bw. Hamad Rajabu Mbega, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi;
(v) Bw. Peter Nicholaus Masindi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu
(vi) Bw. Joseph Josephat Mkude amehamishwa kutoka Wilaya ya Kishapu kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha kuchukua nafasi ya Bw. Felician Gasper Mtahengera ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
(vii) Bw. Joachim Thobias Nyingo amehamishwa kutoka Wilaya ya Kilolo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi;
(viii) Bi. Rebecca Sanga Msemwa amehamishwa kutoka Wilaya ya Bahi kwenda kuwaMkuu wa Wilaya ya Kilolo;
(ix) Bw. Hassan Omary Bomboko amehamishwa kutoka Wilaya ya Ubungo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai;
(x) Bw. Lazaro Jacob Twange amehamishwa kutoka Wilaya ya Hai kwenda kuwa Mkuuwa Wilaya ya Ubungo;
(xi) Bi. Kisa Gwagisa Kasongwa amehamishwa kutoka Wilaya ya Njombe kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Makete;na
(xii)Bw. Juma Samwel Sweda amehamishwa kutoka Wilaya ya Makete kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe.
b) Makatibu Tawala wa Wilaya
(i) Bw. Jacob Julius Rombo amehamishwa kutoka Wilaya ya Mbogwe kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha kuchukua nafasi ya Bw. Khamana Juma Simba ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga;
(ii) Bw. Benard Dominic Urasa, Afisa Tawala Mkuu, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa kuchukuanafasi ya Bw. Michael John Semindu ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu;
(iii) Bw. Paul Francis Faty, Mhadhiri Chuo cha Serikali za Mitaa, Hombolo ameteuliwakuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbogwe kuchukua nafasi ya Bw. Jacob Julius Rombo ambaye amehamishwa kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha;
(iv)Bi.Happyness John Sulle, Mkuu wa Kitengo cha Maktaba na Nyaraka wa Chama chaMapinduzi (CCM) ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama kuchukua nafasi ya Bw. Peter Nicholaus Masindi ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu;na
(v) Bi. Glory Absalum, Afisa Tarafa ya Bashnet, Babati ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama kuchukua nafasi Bw. Hamad Rajab Mbega ambayeameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi.
c)Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
(i) Bw.Edwin Lussa Bayona, Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe kuchukua nafasi ya Bi. Saada Selemani Mwaruka ambaye atapangiwa majukumu mengine;
(ii) Bi. Christina Daniel Bunini, Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu,Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kuchukua nafasi ya Mhandisi Stephano Bulili Kaliwa ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
(iii) Dkt. Mwinyi Omary Mwinyi, Mtakwimu Mwandamizi, Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo;
(iv) Bw. Alphaxard Mashauri Etanga, Meneja wa Maendeleo ya Biashara na Wateja,Benki ya Exim ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
(v) Bi. Erica Epaphras Yegela, aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mji wa Masasi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kuchukua nafasi ya Bw. Paul Sweya ambaye amestaafu;
(vi) Bi. Pili Ramadhani Kitwana, Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu,Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendajiwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara;
(vii) Bi.Zahara Muhidin Michuzi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Ifakara kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kuchukua nafasi ya Bw. Athuman Hamis Masasi ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
(viii) Bi.Loema Isaya Peter amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Busokelokwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kuchukua nafasi ya Bw. Linno Pius Mwageni ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
(ix) Bi. Beatrice Clever Mwinuka amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosakuchukua nafasi ya Bw. Michael John Gwimile ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
(x)Bi. Siwema Hamud Juma amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo;
(xi) Bw. Hassan Juma Mnyika amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba;
(xii) Bw. William Mathew Makufwe amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya yaMakete kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua;
(xiii) Bw. Jerry Daimon Mwaga amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete;
(xiv) Bw. Kastori Msigala amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi; na
(xv) Bw. Justice Laurent Kijazi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ikungikwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
d) Mwenyekiti wa Bodi
(i) Bi.Yokbeth Festo Myumbilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kuchukua nafasi ya Prof. Justinian Rwezaula Ikingura ambaye amemaliza muda wake.