DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Grace Elias Magembe kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Magembe alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na anachukua nafasi ya Prof. Tumaini Joseph Nagu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Vilevile Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe amehamishwa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya.
Rais Samia amemuhamisha pia Dkt. John Anthony Jingu kutoka Wizara ya Afya kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.