DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe.Daniel Godfrey Chongolo, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi? Mhe. Bi. Ester Alexander Mahawe.
Marehemu Mahawe amefariki leo tarehe 14 Januari, 2025 katika hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mahawe mahala pema peponi, Amina.