ZANZIBAR-Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama cha Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye Tanzania ni Mwenyekiti wa kamati hiyo kinafanyika Zanzibar leo Januari 4, 2025.
Kikao hicho kimeitishwa kwa ajili ya kujadili hali ya siasa na usalama nchini Msumbiji kufuatia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Oktoba 9,2024.
Mkutano huo wa Makatibu Wakuu unafanyika chini ya Mwenyekiti, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi, Dkt. Samwel W. Shelukindo. Nchi zinazoshiriki mkutano huo ni mwenyeji Tanzania,Zambia na Malawi.