MBEYA-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akisalimiana kwa njia ya miguu na baadhi ya viongozi mbalimbali wa Jiji la Mbeya tarehe 7 Januari, 2025 ikiwa ni ishara ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu mapambano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.