Sasa kila mwanafunzi ataenda shule-CRDB

DAR-Kupitia mkopo wa ada wa hadi shilingi milioni kumi na mbili (12,000,000) uliozinduliwa leo na Benki ya CRDB na kupewa jina ‘ADA LOAN’ ni mkombozi katika sekta ya elimu nchini kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu.
Mkopo huu unakwenda kusaidia wazazi na walezi na hata wanafunzi kukamilisha malipo ya ada kirahisi wakiwa popote kupitia App ya SimBanking.

Ni kwa wateja wanaopitisha mishahara yao Benki ya CRDB pamoja na wateja wasiopitisha mishahara yao Benki ya CRDB ambao watatakiwa kutoa dhamana zitakazohitajika.

Uzinduzi huu uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mkuu wa Fedha, Benki ya CRDB, Ndugu. Fredrick Nshekanabo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Stephen Adili, wafanyakazi wa Benki pamoja na wageni waalikwa wakiwemo Mahmoud Mringo- Mkurugenzi wa Paradigm schools na mwenyekiti wa TAPIE na wadau mbalimbali waliohudhuria wakiwemo wazazi, walimu, Wakurugenzi wa tasisi za elimu na wanafunzi wa shule.
Benki ya CRDB inaendeleza jadi ya kutoa huduma za kibunifu na rahisi zaidi nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news