DAR-Kocha wa Young Africans SC, Sead Ramovic amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi Desemba akiwashinda Fadlu Davids wa Simba SC na na Rachid Taoussi wa Azam Fc alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za TFF.
Ramovic aliiongoza Yanga kushinda michezo yote minne iliyocheza mwezi huo na kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili kwenye msimamo wa ligi, Yanga Sc ikizifunga Tanzania Prisons mabao 4-0, iliifunga Dodoma Jiji mabao 4-0, Mashujaa mabao 3-2 na Fountain Gate mabao 5-0.