Sekta ya Madini yafanya kweli miaka minne

NA GODFREY NNKO

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema,Serikali imeimarisha sekta ya madini kwa kuweka mazingira wezeshi ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Pia,Serikali imeimarisha miundombinu wezeshi,masoko ya madini na kuwawezesha wachimbaji wadogo.
Waziri Mkuu amesema, kutokana na jitihada hizo katika kipindi cha miaka minne, mmafanikio makubwa yamepatikana ikiwemo kutoa leseni tano kwa kampuni tano.

Miongoni mwa kampuni hizo mi Sotta Mining Corporation Limited (SMCL) wilayani Sengerema,Tembo Nickel Corporation Ltd (TNCL) wilayani Ngara, Faru Graphite Corporation Ltd (FGCL) wilayani Mahenge.

Nyingine ni Mamba Minerals Corporation Limited wilayani Songwe na Nyati Mineral Sand Limited wilayani Pangani ambazo zimeiwezesha Serikali kukusanya shilingi trilioni 2.64.

Ameyasema hayo Januari 19,2025 jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi Desemba,2024.

Ni mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao umeongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Makusanyo ya maduhuli ya Serikali yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 624.61 mwaka 2021 hadi bilioni 753.82 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 20.7."

Waziri Mkuu amesema, mafanikio mengine ni kuanzishwa kwa kiwanda cha kusafisha na kuongeza thamani ya dhahabu cha Geita chenye uwezo wa kusafisha kilo 600 za madini kwa siku.

Pia,kununua mitambo mitano ya uchorongaji wa madini iliyowanufaisha wachimbaji wadogo na kutoa mafunzo kwa wachimbaji 750,348 kuhusu leseni za madini, usalama migodini, utunzaji wa mazingira, masuala ya baruti na biashara ya madini.

Amesema,pia Serikali imetoa leseni 30,191 za uchimbaji mdogo wa madini ikiwemo kuanzisha vituo 65 vya ununuzi wa madini katika mikoa 30 ya kimadini na kufanya jumla ya vituo vya ununuzi wa madini kufikia 105.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news