Serikali yaamuru wafanyakazi Dar kufanyia kazi nyumbani Januari 27 na 28,2025

DAR-Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaotarajiwa kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kuanzia tarehe 27 hadi 28 Januari 2025.
Mkutano huo ambao jumla ya Marais 25 kutoka nchi za Afrika wanatarajiwa kushiriki unatajwa kuwa wa kihistoria ukilenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto na fursa za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la Dar es Salaam, linalosisitiza dhamira ya Viongozi wa Nchi na Serikali za Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news