Serikali yatoa wito kwa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi

ZANZIBAR-Waziri wa Ardhi Nyumba na Makaazi, Mheshimiwa Rahma Kassim Ali amekitaka Kikosi cha Zimamoto na Uokozi kuendelea kuwatumia wataalamu wake wa ndani katika kutekeleza miradi yake ili kupunguza gharama na kuhakikisha fedha zinatumika ipasavyo na kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Ameyasema hayo alipokifungua Kituo cha Zimamoto na Uokozi Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.

Amesema,fedha ambazo zinatumika katika miradi hiyo ni fedha za ndani hivyo ipo haja ya kuthamini mchango wa serikali kwa kuzitumia kwa malengo yaliopangwa.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,Mikidadi Mbarouk Mzee amemema,azma ya Serikali ni kuhakikisha wanajenga vituo vya kisasa vya Zimamoto na Uokozi kila wilaya na kwa sasa wameshajenga vituo viwili Kiwengwa Wilaya ya Kaskazini A na Mkanyageni Wilaya ya Mkoani.
Naye Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi, Rashid Mzee Abdalla amesema,Serikali itaendelea kuwasogezea wananchi wake huduma za kuzima moto na uokozi ili kukabiliana na majanga pindi yanapotokea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news