Simba SC hatuna presha dhidi ya SC Constantine-Kocha Fadlu Davids

DAR-Kocha Mkuu wa Simba Sports Club,Fadlu Davids amesema, pamoja na umuhimu mkubwa uliopo wa kutafuta alama tatu katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya CS Constantine, lakini hawana presha.
Kocha Fadlu amesema itakuwa mechi ngumu kwa kuwa kila moja inahitaji alama ili kujihakikisha kuongoza kundi, lakini hawana presha na wamejipanga kucheza soka safi la kuburudisha.

Akizungumzia hali ya kikosi Fadlu amesema, wachezaji wapo kwenye hali nzuri na morali zipo juu na kila mmoja yupo tayari kupambana kuhakikisha tunawapa furaha Wanasimba.

“Haiwezi kuwa mechi rahisi kwa kuwa tunahitaji kushinda ili kuongoza kundi na wenzetu wanahitaji hata alama moja,lakini hatuna presha tutacheza soka letu tulilolizoea,” amesema Fadlu.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu amesema,wapo tayari kuhakikisha tunapata ushindi na kuongoza kundi ili kuwaburudisha Wanasimba.

Awesu amezungumzia pia kuhusu kukosekana kwa mashabiki kuwa wachezaji wameumia, lakini kupitia dua na maombi mbalimbali wanaamini wataweza kushinda na kupata pointi tatu na kuongoza kundi.

“Sisi tupo tayari na tunajua kwetu ni kama fainali kwa kuwa tunahitaji ushindi ili kuongoza kundi na uwezo huo tunao. Tunahitaji sala na maombi kutoka kwa mashabiki wetu,” amesema Awesu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news