DAR-Simba Sports Club (Simba SC) ya jijini Dar es Salaam inaongoza Kundi A la Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa alama 13.
Ni baada ya kuichapa CS Constantine mabao 2-0 katika mtanange ambao umepigwa leo Januari 19,2025 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ulikua wa kuhitimisha hatua ya Makundi mabao ya Simba SC yamefungwa na Kibu Denis dakika ya 61 na Leonel Ateba dakika ya 79.
Aidha, nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi A inashililiwa na CS Constantine yenye alama 12.Kundi hilo pia lina timu za Bravos FC ambayo ina alama 7 na CS Sfaxien yenye alama 3.