Simba SC mguu kwa mguu dhidi ya CS Constantine leo

DAR-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam leo Januari 19,2025 saa 10 jioni itashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili CS Constantine kutoka Algeria.
Ni katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Huu,utakuwa mchezo mgumu ambao utaamua nani atakuwa kinara wa kundi baina ya Simba SC na CS Constantine.

Pamoja na Simba SC kufuzu robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, lakini leo wanahitaji kushinda ili kuwa vinara wa kundi.

Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema,pamoja na ukubwa na umuhimu wa mchezo wenyewe ambao kila timu inahitaji alama tatu, lakini hawatacheza kwa presha.

Fadlu amesema,watacheza soka lao walilolizoea, lakini kwa kuchukua tahadhari zote kwa kuwa jambo muhimu ni kuhakikisha wanapata alama zote tatu.

“Haiwezi kuwa mechi rahisi kwa kuwa tunahitaji kushinda ili kuongoza kundi na wenzetu wanahitaji hata alama moja, lakini hatuna presha tutacheza soka letu tulilolizoea,” amesema Fadlu.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu amesema wapo tayari kuhakikisha tunapata ushindi na kuongoza kundi ili kuwaburudisha Wanasimba.

Awesu amezungumzia pia kuhusu kukosekana kwa mashabiki kuwa wachezaji wameumia lakini kupitia dua na maombi mbalimbali wanaamini wataweza kushinda na kupata pointi tatu na kuongoza kundi.

“Sisi tupo tayari na tunajua kwetu ni kama fainali kwakuwa tunahitaji ushindi ili kuongoza kundi na uwezo huo tunao. Tunahitaji sala na maombi kutoka kwa mashabiki wetu,” amesema Awesu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news