DAR-Klabu za Simba na Young Africans Sports Club (Yanga SC) za jijini Dar es Salaam zimeendelea kuipeperusha vema bendera ya Tanzania katika anga za Kimataifa baada ya kupanda viwango vya ubora barani Afrika.
Simba Sports Club baada ya kutinga kibabe katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na kuongoza katika kundi lake mbele ya klabu za CS constantine ya Algeria,Bravos ya Angola na Cs Sfaxien ya Tunisia imepanda viwango vya ubora wa vilabu barani Afrika hadi nafasi ya sita kutoka nafasi ya saba baada kuishusha Rs Berkane ya nchini Morroco.
Kwa upande wa Yanga SC wamefanikiwa kupanda hadi nafasi ya 10 kutoka nafasi ya 13 ambayo walikuwa awali baada ya kuzishusha klabu za Raja Casablanca,Tp Mazembe na Petro Atletico.