Simba SC yatinga robo fainali Kombe la Shirikisho barani Afrika

LUANDA-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imetinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup).

Hatua hiyo wameifikia leo Januari 12,2025 katika Dimba la Estádio 11 de Novembro lililopo mjini Luanda, Angola baada ya sare ya kufungana dhidi ya Futebol Clube Bravos do Maquis (Bravos do Maquis).
Ni katika mchezo wa tano wa hatua ya makundi ambao umeifanya Simba SC kufuzu moja kwa moja hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Abednigo Mosiatlhaga aliwapatia wenyeji bao la mapema dakika ya 13 kufuatia mlinzi wa kati Che Fondoh Malone kurudisha pasi fupi ambayo iliunganishwa na mfungaji huyo.

Baada ya bao hilo,Simba SC waliongeza kasi ya mashambulizi ili kutafuta bao la kusawazisha ingawa ufanisi wao mbele ya lango la Bravos haukuwa mzuri.

Leonel Ateba awapatia bao la kusawazisha dakika ya 68 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi Shomari Kapombe.

Ushindi huu umeifanya Simba kufikisha alama 10 wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi A huku tukisalia na mechi moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news