MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge ya Mfuko wa Elimu Na. 8 ya 2001 chini ya kifungu cha 5 (1)ili kuratibu na kusimamia Mfuko wa Elimu,ulioanzishwa kwa sheria hiyo hiyo.
Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2013.Madhumuni ya Mfuko wa Elimu ni kuongeza nguvu za Serikali katika kugharamia miradi ya elimu ili kuinua ubora wa elimu na upatikanaji wake kwa usawa, katika ngazi zote za Elimu kwa Tanzania Bara na Elimu ya Juu kwa Tanzania Zanzibar.
MFUKO WA ELIMU
Mfuko wa Elimu unapokea rasilimali fedha na vifaa ambazo hukusanywa na kuratibiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa lengo la kufadhili miradi ya elimu nchini kutoka vyanzo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
TEA imepewa jukumu la kuhamasisha wadau mbalimbali nchini na nchi za nje kuchangia rasilimali mbalimbali kwa lengo la kusaidia juhudi za Serikali kuinua ubora, na kuongeza upatikanaji wa elimu kwa usawa.
Dira
Kuwa Mfuko wa Elimu bora, wenye hadhi ya kimataifa, unaotatua changamoto za elimu nchini, kwa kutumia vyanzo mbalimbali vyamapato katika kuchangia maendeleo endelevu nchini.
Dhamira