DODOMA-Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema kufuatia taarifa ya Serikali kuhusu agizo la baadhi ya Watumishi wa Umma kufanyia kazi nyumbani, Wizara hiyo inaelekeza Shule zote za Msingi, Sekondari na Vyuo katika Mkoa wa Dar es Salaam kufungwa kwa siku mbili Januari 27 na Januari 28, 2025.
Taarifa iliyotolewa leo Januari 26,2025 na Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa imesema “Tangazo hili ni kwa Vyuo na Shule za Serikali na Binafsi, Wadau wote wa elimu wanaombwa kuzingatia tangazo hili ili kuepusha changamoto za usafiri zinazoweza kujitokeza kutokana na kufungwa kwa baadhi ya barabara, masomo yataendelea kama kawaida kuanzia January 29, 2025”