DAR-Katika kuboresha ufanisi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),Taasisi ya Uongozi imetoa mafunzo ya siku mbili kwa Bodi ya TMA.Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Bodi Mh.Jaji Mshibe Ali Bakari katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF Jengo la Millenium II jijini Dar es Salaaam tarehe 29 hadi 30 Januari 2025.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mh, Jaji.Mshibe alisema “Jambo muhimu katika mafunzo haya ni kuimarisha ushirikiano na uwazi ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi kwenye Taasisi yetu.’’
Katika hatua nyingine,Bodi hiyo ilifanya ziara ya kutembelea mradi wa ofisi ya Kanda ya Mashariki na kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Tsunami,ambapo Katibu wa Bodi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi,Dkt.Ladislaus Chang’a aliishukuru Bodi, kwa kutembelea eneo la mradi na kwa maelekezo na miongozo ya kuhakikisha kuwa mradi unafanyika kwa ufanisi.
Mafunzo hayo yamejumuisha Bodi na Menejimenti ya TMA ambapo mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo uongozi bora,uongozi wa kimkakati na vihatarishi vinavyoweza kukwamisha ufanisi wa Taasisi.
Tags
Habari
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Taasisi ya Uongozi
Tanzania Meteorological Agency (TMA)