TAKUKURU na MISA TAN kushirikiana mapambano dhidi ya rushwa nchini

DODOMA-Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini Mwa Afrika - Tawi la Tanzania (MISA Tan) Bw. Edwin Soko, amemtembelea Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Crispin Francis Chalamila - Januari 20, 2025.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika TAKUKURU MAKAO MAKUU jijini Dodoma, yalilenga kuimarisha ushirikiano katika kuelimisha na kuhabarisha masuala dhidi ya Rushwa pamoja na kuwashirikisha waandishi wa habari kwenye utekelezaji wa Programu ya TAKUKURU RAFIKI.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu amepongeza hatua ya MISA Tan kutaka kushirikiana na TAKUKURU katika jitihada za kuzuia Rushwa na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo kwani wadau wa habari wana wigo mpana wa kufikisha habari kwa wananchi.

Mazungumzo hayo yamefanyika ikiwa ni mwendelezo wa uongozi mpya wa Bodi ya MISA Tan ya kuwatembelea wadau mbalimbali kwa lengo la kujitambulisha na kupanua wigo wa kufanya kazi na wadau hao wakiwemo TAKUKURU.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news