Tanzania itaendelea kuwa nchi ya kutegemewa duniani-Rais Dkt.Samia

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuwa nchi ya kutegemewa katika kukuza ushirikiano wa kimataifa, kuchochea ukuaji wa kiuchumi, na kudumisha amani na usalama barani Afrika na duniani kwa ujumla.
Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025.

Rais Dkt.Samia ameyasema hayo wakati wa hafla maalum aliyoiandaa kwa ajili ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa yaliyopo nchini.

Hafla hiyo huandaliwa kila mwanzo wa mwaka kutakiana heri, kuzungumzia maendeleo nchini nakueleza vipaumbele vya Tanzania ikiwemo kikanda na kimataifa.
Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025.

Pamoja na mambo mengine, Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa pamoja na kuadhimisha miaka 60 ya Muungano, mwaka 2024 Tanzania ilishuhudia ukuaji wa kiuchumi wa asilimia 5.4 ambao umechagizwa na kukua kwa uzalishaji, uwekezaji na utalii.

Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa nchi ilipiga hatua za kihistoria katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya reli na nishati inayoenda kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini Tanzania.

Aidha, Rais Dkt. Samia amebainisha kuwa mwaka 2025 Tanzania itakamilisha maandalizi ya Dirampya ya Maendeleo ya Taifa na mapitio ya Sera ya Mambo ya Nje; nyaraka zitakazobainishavipaumbele vya nchi na zitakazoongoza pia ushirikiano kati ya Tanzania na wabia wake.
Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025.
Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) Ikulu ǰijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025.

Kimataifa, Tanzania inakusudia kuendelea kuimarisha mahusiano na wabia wake na kukuzamahusiano kwenye sekta muhimu za maendeleo ikiwemo elimu, afya na nishati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news