Tanzania kuanza kuzalisha kompyuta

DODOMA-Tanzania iko mbioni kuwa na kiwanda kikubwa cha kutengeneza kompyuta mpakato (Laptop) kitakachozalisha kompyuta aina ya Tanzanite.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya taasisi yake mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu jana bungeni jijini Dodoma.

Aidha, nyingi ya komyuta hizo zitaelekezwa katika kukuza sekta ya TEHAMA kuanzia shule za msingi hadi sekondari.

Hayo yalibainika Bungeni jijini Dodoma jana wakati Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga alipofanya wasilisho juu ya tume yake mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, chini ya Mwenyekiti wake, Moshi Kakoso.

Mwasaga alisema mafanikio hayo yanatokana na juhudi za Serikali kupitia Tume ya TEHAMA katika kuvutia uwekezaji na ujenzi wa vifaa vya TEHAMA nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu, Mh. Moshi Kakoso (kulia) akifuatilia wasilisho la utekelezaji wa majukumu ya Tume ya TEHAMA jana bungeni jijini Dodoma. Wasilisho hilo lilifanywa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga aliyeshuhudiwa na viongozi wakuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, wakiongozwa na Waziri wake, Mhe. Jerry Silaa.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya taasisi yake mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu jana bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mh. Jerry Silaa akifafanua jambo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Tume ya TEHAMA bungeni jana mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyoketi chini ya uenyekiti wa Mhe. Moshi Kakoso.
Viongozi wakuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakiongozwa na Waziri, Jerry Silaa wakifuatilia wasilisho la taarifa ya utekelezaji wa Tume ya Tehama lililowasilishwa bungeni Dodoma jana mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu. Wengine pichani ni Naibu Waziri, Maryprisca Mahundi (kushoto), Katibu Mkuu wa wizara, Mohammed Khamis Abdulla na Naibu Katibu Mkuu, Nicholas Mkapa.

“Tuko pazuri. Tume imeshaitembelea kampuni ya QuadGen Wireless Solutions Pvt. Ltd ya Bangalore, India ili kujionea uwezo wao baada ya kampuni hiyo kuonesha utayari wa kuwekeza kiwanda kitakachotengeneza kompyuka mpakato na mfumo wa ubao janja kwa ajili ya kufundishia shule.

“Tume inaendelea na mazungumzo na kampuni hii ili kuwezesha uwekezaji wa ubia wa viwanda vya viwango vya SKD (kiwanda cha kuunda) na CKD (kiwanda cha kutengeneza) nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya taasisi yake mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu jana bungeni jijini Dodoma.

"Hii inaendana na shabaha iliyowekwa na Umoja wa Afrika kwa bara letu kuwa na viwanda vya kutengeneza bidhaa za TEHAMA,” alisema Dkt. Mwasaga.
Hatua hiyo ilipongezwa na Kamati na kuisihi Tume ya TEHAMA kuongeza kasi katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kuwa kama nchi, macho yote kwa sasa yapo katika mwelekeo wa kuujenga uchumi wa kidigitali kupitia kundi kubwa la vijana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Mhe. Moshi Kakoso alipongeza na kusisitiza kuwa, fursa kama hizo hazipaswi kuachiwa, bali zifanyiwe kazi ziweze kunufaisha nchi.

Alisema makosa kadhaa yalifanyika miaka ya nyuma baada ya wawekezaji kutaka kuzalisha bidhaa nchini, lakini wakaishia kuhamia nchi jirani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news