SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) limepanga makundi ya fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zinazofanyika Desemba mwaka huu nchini Morocco.
Droo hiyo imeshirikisha timu 24 zilizofuzu kwenye makundi sita kila moja likiwa na pande nne kwa ajili ya fainali hizo zinazotarajiwa kuanza Desemba 21,2025 hadi Januari 18 2026.
Tanzania imepangwa kundi C pamoja na Nigeria, Tunisia na Uganda. Kundi A : Morocco, Mali, Zambia, Comoros. Kundi B: Misri, Afrika Kusini, Angola na Zimbabwe. Kundi D: Senegal, DR Congo, Benin na Botswana.
Kundi E: Algeria, Bukna Faso, Equatorial Guinea na Sudan. Kundi F: Ivory Coast, Cameron, Gabon na Msumbiji.