TRC yaomba radhi kwa abiria

DAR-Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa pole kwa abiria waliokuwa wakisafiri kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma Januari 8, 2025 kufuatia usumbufu uliojitokeza kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea katika Kituo cha lhumwa jijini Dodoma majira ya saa 5:38 usiku.
TRC imesema inajua safari za kawaida kati ya Dar es salaam na Dodoma zimeathirika na hii inawezakuwa na athari kubwa kwa abiria.

“Mafundi wetu wamepambana kurekebisha tatizo husika na kuhakikisha huduma zetuzinarejea kwenye hali ya kawaida, treni zilizoathirika ni treni iliyoondoka saa 12.55 jioni siku ya Jumanne Januari 7, 2025 kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma iliyotarajiwa kufika 5.01 usiku badala yake ilifika saa 7 usiku, treni inayoondoka saa 11.15 asubuhi siku ya Jumatano Januari 8, 2025 kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam iliondoka saa 3.05 asubuhi.

"Treni iliyotakiwa kuondoka saa 12.00 asubuhi Januari 8, 2025 kutoka Dar es Salaam kueleka Dodoma iliondoka saa 12.30 asubuhi na treni iliyotakiwa kuondoka saa 3.30 asubuhi sikuya Jumatano Januari 8, 2025 imeondoka saa 11.55 kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma.Shirika linaendelea kuomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news