NA DEREK MURUSURI
Januari 10, 2025
MWENYEKITI wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi Joyce Mapunjo ameihakikishia Menejimenti ya Mfuko huo ushirikiano wake ili kufikia malengo ya Mfuko huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi Joyce Mapunjo, akiongea na Wakurugenzi na Mameneja wa Mfuko huo, katika retreat iliyofanyika Kibaha, Pwani, hivi karibuni.
Bi Mapunjo alikuwa anaongea katika mkutano wake wa kwanza na Wakurugenzi na Mameneja wa Mfuko huo, mwanzoni mwa wiki hii, baada ya kuteuliwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PSSSF, tarehe 2 Disemba, 2024.
“Niwahakikishie kuwa tutafanya vizuri, niko transparent na huwa sipendi majungu,” alisema na kuipongeza Menejiment ya Mfuko huo kwa kuwakutanisha Wakurugenzi pamoja na Mameneja wao, kwa mara ya kwanza toka Mfuko huo uanzishwe mwaka na Sheria ya Hifadhi ya Jamii Kwa Watumishi wa Umma ya Mwaka 2018, wakakaa pamoja na kupitia mipango na bajeti zao pamoja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi Joyce Mapunjo, akiongea na Wakurugenzi na Mameneja wa Mfuko huo, katika retreat iliyofanyika Kibaha, Pwani, hivi karibuni.
Walijifungia kwa siku nne (4) ili kufanya mapitio ya utekelezaji wa mipango ya miezi sita iliyopita na kuweka mikakati ya utekelezaji wa mipango mingine ya miezi sita ijayo, ikiwa ni pamoja na kuasisi mipango ya mabadiliko.
“Mkapa alikuwa anakwambia tafuteni stakeholders [wadau] na tulikuwa tunawatafuta wapinzani ili watuambie wapi tunahitaji kuboresha. “Retreat ijayo muwa identify [wachague] stakeholders [wadau] na wakaribisheni katika retreat kama hii ili waongee.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw Abdul-Razaq Badru.
Alisema taasisi zilizofanikiwa ni zile ambazo zilikuwa zinakutana na wadau wao mara kwa mara, “…kama mtawala, organizations [taasisi] zilizokuwa zinafanya vizuri, ni zile ambazo zilikuwa zinafanya interactions [zinajichanganya] na wadau wao.
Katika Kanda ya Mashariki, Morogoro, Mfuko umekuwa unakutana na Wadau hadi katika Tarafa na elimu imetolewa na changamoto za Wateja na Wadau wao kutatuliwa.
“Tumepokea maelekezo hayo kutoka kwa Mwenyekiti wetu na tunaanza kuyafanyia kazi mara moja ikiwa ni pamoja na kuongeza juhudi kwenye huduma za outreach, [kuwatembelea] kwa wadau wetu na kuendelea kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii,” alisema Bw Abdul-Razaq Badru, katika mahojiano baada ya hafla hiyo.
Bi Mapunjo alimpongeza Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti ya PSSSF kwa kikao kazi [retreat] kinachoasisi mpango wa mabadiliko na kusema kuwa alijisikia vizuri sana kuanza majukumu yake kwenye Mfuko huo katika kipindi muhimu cha kuanza safari ya mabadiliko ya kuuboresha Mfuko.
Wakurugenzi na Mameneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wakiendelea na majadiliano ya kuasisi safari ya mabadiliko PSSSF wiki hii, Kibaha Mkoani Pwani.
Mwezeshaji Mtanzania anayeishi na kufanya shughuli zake nchini Marekani, Dennis Massawe, naye amempongeza DG Abdul-Razaq Badru kwa kukaa takriban siku 4 na Wakurugenzi na Mameneja wake wakijadili pamoja kazi zilizofanyika na kuweka mikakati ya kuwezesha safari ya mabadiliko ili kuboresha huduma za Mfuko huo.
PSSSF imedhamiria kuwa “agile organization,” yaani taasisi inayochakata madai na maombi mbalimbali ya wateja wake kwa haraka na kwa ufanisi ili wateja na wadau wake waweze kupata majibu yao kwa wakati na kuboresha maisha yao.
Kikao kazi hicho cha kuasisi mabadiliko hayo, kinafanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, inayomilikiwa na vyama vitano vya ukombozi vya Kusini mwa Afrika, kilichopo Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF Joyce Gideon Mapunjo (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Abdul-Razaq Badru (kushoto) na Mbaruku Magawa, Mkurugenzi wa Uendeshaji (kulia) wakifuatilia majadiliano katika retreat ya Kibaha Story 2025.
Madhumuni ya Retreat ya Kibaha Story 2025
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF Bw Abdul-Razaq Badru, alisema madhumuni ya retreat hiyo ilikuwa ni kufanya mapitio ya utendaji kazi wao katika kipindi cha miezi sita (6) iliyopita na kukubaliana vipaumbele vya miezi sita ijayo, ikiwa ni pamoja na maandalizi ya safari yao ya mageuzi na mabadiliko.
Aliendelea kusema kuwa mabadiliko hayo yataifanya PSSSF kuimarisha uwezo wake na kuendelea kuwa kitaasisi endelevu na yenye kutoa mafao bora zaidi kwa Wastaafu wake wa sekta ya umma ikiwa ni katika kutafsiri maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Bw Badru alisema mabadiliko haya pia yanalenga kuimarisha utendaji bora zaidi wa Mfuko, kuangalia fursa nyingine mbalimbali ambazo Mfuko unaweza kuzitumia ili kukidhi matarajio ya wadau wake.
Safari hiyo ya kuasisi mabadiliko, ambayo kwa ubunifu mkubwa wameipa jina la “Kibaha Story 2025,” inaangalia mageuzi yanayohitajika ndani ya taasisi ili kuweza kuwa na Mfuko endelevu na unaotoa huduma bora zaidi kwa Wanachama wa Mfuko na Wastaafu nchini, katika kutafsiri maono ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, imekuwa mwanzo mzuri na kimsingi ni mafanikio makubwa ya safari hiyo.
“It is a new beginning at PSSSF (ni mwanzo mpya PSSSF), ambapo Mkurugenzi Mkuu, Wakurugenzi na Mameneja wote wanakaa pamoja, kwa mara ya kwanza (toka PSSSF ianzishwe kwa mara ya kwanza mwaka 2018), katika historia ya taasisi, kufanya mapitio ya utendaji kazi wao kwa pamoja na kuweka vipaumbele na mikakati ya kufanya vizuri zaidi katika siku za usoni,” alisema Bw Dennis Massawe, ambaye ni mmojawapo wa Wawezeshaji.
Mwandishi wa makala hii ni Mtaalam wa mawasiliano, biashara, menejimenti, habari na mwandishi wa vitabu. Anapatikana kwa +255 787 17 67 67.