ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameendelea kuwahimiza wananchi umuhimu wa kuitunza amani iliyopo nchini kwa lengo la kuleta maendeleo zaidi.
Alhaji Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipojumuika na waumini wa dini ya Kislamu wa Masjid Sunni Hanaf Mkunazini katika Sala ya Ijumaa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Alhaj Dkt.Mwinyi amewakumbusha waumini hao kuiombea nchi amani wakati huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu.
Amesisitiza kuwa, ni vema waumini na wananchi wakaondoa tofauti zao za kidini,kisiasa na kijamii na kuweka mkazo kuiombea nchi amani kwani bila amani hakuna maendeleo.
Baada ya Ibada hiyo ya Sala ya Ijumaa Alhaj Dkt.Mwinyi alitembelea Maskani ya Jaws Corner ya Mji Mkongwe kuwasalimia wakazi wa eneo hilo na kupata fursa ya kuzungumza nao na kutunukiwa zawadi na wananchi hao.
Aidha,alitembelea Maskani ya Lebanon Brother na kupokelewa kwa furaha na wakazi wa hapo.
Alhaj Dkt.Mwinyi amekuwa na Utaratibu Maalum wa kuwatembelea wananchi na kuwafariji wagonjwa katika maeneo mbalimbali hususan baada ya kukamilisha Ibada ya Sala ya Ijumaa.