Tumevuka lengo la Ilani ya Uchaguzi ujenzi barabara za lami-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema,Serikali imevuka lengo la Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 ilioainisha ujenzi wa kilomita 275 za barabara.
Ameeleza kuwa, Serikali imeamua kuongeza idadi ya barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami hadi kufikia kilomita 300 Mijini na Vijijini.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipoifungua Barabara ya Ukutini hadi Bandarini Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo Januari 10, 2025.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amesema,mkataba wa wananchi na Serikali yao ni Ilani ya Uchaguzi hivyo kuna kila sababu ya kujivunia kwa yote yaliofanyika katika ujenzi wa barabara.

Akizungumzia barabara ya Ukutini hadi Mtangani Bandarini aliyoifungua amesema, ni hatua muhimu ya kufungua fursa za kiuchumi.

Ameeleza kuwa,mbali na usafiri barabara hiyo ya Ukutini hadi Bandarini itafungua fursa za ajira kwa kuwa, kuna Bandari na Hoteli katika eneo hilo pamoja kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijami ikiwemo Hospitali, Skuli na Usafirishaji.

Ufunguzi wa Barabara hiyo kunakamilisha idadi ya kilomita 85.5 za barabara zilizojengwa katika Mkoa wa Kusini Pemba.
Barabara ya Ukutani - Bandarini yenye urefu wa kilomita 4.6 iliyojengwa na Kampuni ya IRIS na kugharimu dola Milioni 2.658 ni miongoni mwa Mradi wa Ujenzi wa Barabara za ndani zenye urefu wa kilomita 275.9.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news