DAR-Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amemteua John Mnyika kuendelea kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, nafasi aliyokuwa akiishikilia tangu Freeman Mbowe alipokuwa mwenyekiti.
Vilevile,Lissu amemteua Wakili Ally Ibrahim Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar), akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Salum Mwalimu aliyeondolewa.
Pi, Amani Golugwa aliyekuwa meneja kampeni wa Lissu katika uchaguzi mkuu wa 2020, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara), akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Benson Kigaila ambaye naye ameondolewa.
Wajumbe wa Kamati Kuu
1. Godbless Lema
2. Dkt. Rugemeleza Nshala-Mwanasheria Mkuu wa Chama
3. Rose Mayemba
4. Salma Musa Kasanzu
5. Hafidh Ally Salehe