Urais wa Zanzibar, CCM ni Dkt.Mwinyi 2025

DODOMA-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Mkutano Mkuu Maalum wa CCM , uliofungwa rasmi na Mwenyekiti wa CCM Taifa , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan tarehe 19 Januari 2025 katika Ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Aidha, Dkt.Mwinyi amethibitishwa na Mkutano huo Mkuu Maalum kuwa Mgombea wa Urais pekee wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi mkuu mwaka huu.
Vilevile, Mkutano huo umemchagua Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea pekee wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM na Dkt.Emmanuel John Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news