Utekelezaji wa mambo ya Muungano umeleta mafanikio makubwa-Waziri Masauni

DODOMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesema usimamizi makini wa utekelezaji wa Mambo ya Muungano umeleta mafanikio katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Amesema yaliyopatikana yaliyopatikana ni kuimarika kwa utaifa na umoja, amani na utulivu na hali ya maisha ya wananchi kutokana na ukuaji wa uchumi wa pande zote mbili za Muungano.

Mhandisi Masauni amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kuanzishwa kwa Akaunti ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mchakato wa kuundwa kwa Tume ya kusimamia akaunti hiyo kwenye Kamati ya kudumu ya Bunge ya kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa Mambo ya Muungano kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yale yasiyo ya Muungano unakwenda sanjari na mipango, sera, programu na mikakati ya maendeleo ambayo Serikali zote mbili zimejiwekea kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa Watanzania.

“Ili kuwa na tija katika utekelezaji na kusogeza huduma karibu na wananchi wa pande zote mbili za Muungano, Serikali imehakikisha Taasisi za Muungano zinajenga au kufungua Ofisi Tanzania Bara na Zanzibar. Taasisi hizo zimekuwa zikitekeleza majukumu yake Zanzibar kupitia utaratibu wa mashirikiano na Taasisi za Zanzibar zenye kufanana katika majukumu,” amesema.

Aidha, Mhandisi Masauni amesisitiza kuwa Taasisi zote za Muungano zinatakiwa kuwa na Ofisi Zanzibar, hivyo Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kuzielekeza ambazo hazijafungua Ofisi Zanzibar ili kusogeza huduma karibu na wananchi wa Zanzibar.

Katika hatua nyingine, amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zinaendelea kushughulikia suala la ufunguaji wa Akaunti ya Fedha ya Pamoja ili kuhakikisha masuala ya mgawanyo wa fedha yanaratibiwa na kusamimiwa kwa ufanisi kwa faida ya pande zote mbili za Muungano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news