DAR-Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Tanzania (ICTC), Dkt. Nkundwe Mwasaga amesema,baada ya mwaka 2050, Tanzania yote itakuwa ya Kidijitali kutokana na vijana wengi wa sasa kuchangamkia fursa za simu janja.
Dkt.Mwasaga ameyasema hayo kupitia mahojiano maalum na Clouds TV wakati akiangazia fursa mbalimbali zilizopo katika teknolojia ya Kidijitali.
"Lakini, wote ninadhani mnafahamu kabisa katika hao uliowasema 60 na, kuna watoto wadogo ambao wapo ambao hawatumii simu. Ukiowaondoa hao, utakuta waliobaki kuwa na simu janja ni wachache sana,
"Kwa sababu sisi, tunatambua vizuri sana, watoto ambao wamezaliwa ukiwachukua mpaka miaka 34 ni asilimia karibu 70.
"Kwa hiyo, wale walioazaliwa mpaka miaka 17 ambao simu kwao ni mzigo ukiwatoa wale, hiyo asilimia uliyoitaja imebaki asilimia ndogo sana ya watu kuwa na simu janja.
"Tatizo la asilimia haioneshi picha kamili, siyo asilimia 36 ya watu wazima, ni asilimia 36 ya watu wote.Lakini, kuna watoto ambao hawana simu...kuna wazee. Ninachowasifu vijana, wengi wamechukua hii fursa na wengi wana simu janja.
"Sasa, wale ndiyo tunasema kijana yeyote ambaye ana umri wa miaka 34 sasa hivi baada ya 2050 atakuwa na miaka 60.
"Kwa hiyo, baada ya 2050, Tanzania yote itakuwa ya Kidijitali kwa sababu hawa watakuwa ni watu wazima, watoto wao watakuwa na hizi teknolojia;