DAR-Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga amesema kuwa, mitandao ya kijamii ikitumika ipasavyo ni fursa kubwa ya ajira na biashara kwa Watanzania.
Ameyabainisha hayo wakati akizungumza katika Kipindi cha Twende Pamoja cha runinga ya Channel Ten jijini Dar es Salaam.
"Itolewe elimu kwa kiasi kikubwa ili watu waweze kutambua ni namna gani ya kuweza kutumia mitandao kwa ubora wake.
"Kwa sababu mitandao kwa sisi tunavyoiona ni fursa, ni fursa ambayo watu wanaweza kuitumia kufanya shughuli zao za kibiashara akapata kipato kizuri na vilevile akaweza hata kuajiri watu wengine;