DAR-Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA nchini,Dkt.Nkundwe Mwasaga amesema,kwa sasa Serikali ipo katika mkakati wa kuangalia ni namna gani shughuli za kila siku nchini zinaguswa na uchumi wa kidijitali ili kufanya maboresho kwa matokeo chanya zaidi.
Dkt.Mwasaga ameyasema hayo katika Kipindi cha Twende Pamoja cha runinga ya Channel Ten jijini Dar es Salaam.
"Watu wengi wamekuwa wakichang'anya kuhusiana na maana halisi ya uchumi wa kidijitali, tuna uchumi wa kawaida ambao tumekuwa tukiujenga tangu tulipopata uhuru ambao wenye unaonekana kwa shughuli za kawaida tunazozifanya.
"Lakini, kwa sasa hivi hasa kuanzia mwaka 2003 pale,tumeanza kuona kuna shughuli zingine ambazo tulikuwa tunazifanyia katika uchumi wa kawaida zinaanza kutumia mifumo ya kidigitali katika kufanya shughuli hizo.
"Moja wapo ni miamala, sasa ukianza kutumia mifumo katika shughuli zile ambazo ulikuwa ukizifanya mwanzo au labda ni shughuli mpya,umeanza kuingia katika uchumi wa kidijitali;