DAR- Idara ya Uhamiaji imetoa taarifa kuhusu Wachezaji Watatu wa Timu ya Singida Black Stars inayoshiriki Ligi Kuu Bara, kuwa wamepewa uraia wa Tanzania baada ya kuomba
Wachezaji hao ni Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana), Josephat Arthur Bada (Cote d’Ivoire) na Muhamed Damaro Camara (Guinea)
Taarifa ya Uhamiaji imeeleza wahusika waliomba kupewa uraia kwa mujibu wa Vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357 na kuwa maombi yao yamekubaliwa na ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi