Wakili Mbedule ataka wananchi Ikuvilo kuhakiki taarifa zao

IRINGA-Wananchi wa Kijiji cha Ikuvilo kata ya Luhota wilaya ya Iringa Vijijini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zao ili waweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Hayo yamesemwa na mdau wa maendeleo na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wakili Sosten Mbedule mara baada ya kuhakiki taarifa zake.

Amesema, ni vema kila mwananchi kuhakiki taarifa zake ili aweze kutumia haki zake za msingi kuchagua viongozi wanaowataka.

"Wananchi wa kijiji cha Ikuvilo wanatakiwa kutumia fursa hii, kwenda kwenye kituo cha kupiga kura na kuhakiki taarifa zake, kuepuka usumbufu hapo badae.

"Wale ambao kadi zao zimeharibika au kupotea ofisa uchaguzi atawasaidia taratibu za kufanya ili wapate kadi mpya,"amesema Wakili Mbedule.

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba 2025, wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news