Waliokaidi ukaguzi magari ya shule Arusha kuchukuliwa hatua

ARUSHA-Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha kimesema kinaendelea na ukaguzi wa magari ya shule maarufu School Bus kwa lengo la kubaini changamoto na ubovu wa magari hayo, huku likibainisha kuwa litawachululia hatua za kisheria wamiliki na madereva wa ambao hawataleta magari kwa ajili ya ukaguzi.
Akiongea wakati wa ukaguzi wa magari hayo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amebainisha kuwa ukaguzi huo ulianza disemba mwaka jana mara baada ya wanafunguzi kufunga shule ili kuondoa usumbufu wanafunzi kipindi cha masomo.

SSP Zauda ameongeza kuwa ukaguzi hu oni kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani kifungu cha 39 sura 168 kama ilivyofanyiwa mapitio 2002 ambapo amewataka wamili na madereva kujitokeza katika zoezi hilo la ukaguzi wa vyombo vya moto kutokana na muda mchache uliobaki.

Pia akasisitiza kuwachukulia hatua za kisheria wamiliki na madereva wote watakao kaidi kufanya ukaguzi wa magari ya shule kwa muda uliobaki sambamba na wale waliobainika vyombo vyao kuwa na changamoto wametakiwa kufanya marekebisho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news